Ufahamu
Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma. Ufahamu wa Kusikiliza Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe. Kujibu Maswali ya Ufahamu kutokana na Habari uliyoisikiliza Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha: Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa. Katika ufahamu wa kusikiliza, msi