Posts

Showing posts from July, 2022

Ufahamu

  Ufahamu ni dhana inayorejelea kujua na kulielewa jambo kwa usahihi na kuweza kulielezea upya kwa usahihi bila kupoteza maana yake ya msingi. Ufahamu wa mtu waweza kupimwa katika kusikiliza jambo au katika kusoma. Ufahamu wa Kusikiliza Ufahamu wa kusikiliza ni zaidi ya kusikiliza tu kile kilichosemwa; badala yake ni uwezo wa mtu kuelewa maana ya maneno anayoyasikia na kuweza kuhusiana nayo kwa namna fulani. Kwa mfano mwanafunzi anaposikiliza hadithi, ufahamu mzuri wa kusikiliza humsaidia kuielewa hadithi hiyo, kuikumbuka, kuijadili, na hata kuisimulia tena kwa maneno yake mwenyewe. Kujibu Maswali ya Ufahamu kutokana na Habari uliyoisikiliza Ufahamu wa kusikiliza unahusisha michakato kadhaa katika kuelewa na kupata maana ya kile kinachozungumzwa. Michakato hii inahusisha: Kuelewa vizuri sarufi ya lugha ile inayozungumzwa Kuelewa vyema maana ya maneno ya mhusiaka anayezungumza Kuelewa sintaksia (muundo wa maneno) ya sentensi kwa namna zinavyowasilishwa. Katika ufahamu wa kusikiliza, msi

Usimulizi | Kiswahili Kidato cha Pili

  Usimulizi ni jumla ya maelezo yanayotolewa na mtu au watu wengi kuhusu tukio fulani. Tukio hilo linaweza kutokea katika wakati mfupi uliopita au zamani kidogo. TUKIO LA MZEE NA KONDAKTA Jana nikiwa nimepanda daladala, kulitokea tukio la Mzee na kondakta wa daladala. Tukio hili lilitoka muda wa saa sita mchana. Kondakta alimfuata Mzee na kumwomba ampe nauli, Yule mzee alidai kuwa, nauli alilipa. Kondakta alidai kama mzee amelipa basi aoneshe tikiti yake. Mzee alidai kuwa, alipotoa fedha, hakupewa tikiti. Pia, mzee alitetewa na watu wengi ambao walidai walishuhudia akilipa nauli. Hata hivyo, kondakta alibaki katika msimamo wake uleule wa kumtaka Mzee alipe nauli au aonyeshe tikiti. Baada ya usumbufu kuwa mkubwa, mzee alisimama akakunja ngumi, konda naye akakunja. Mzee akarusha ngumi nzito, loooh! Konda alianguka mpaka chini. Dereva  alikuja kusaidia, hata hivyo Mzee alikuwa imara, dereva alipigwa ngumi ya kichwa akadondoka hatua mbili alipodondoka konda. Dereva na konda walilala chini

Uandishi | Kiswahili Kidato cha Pili

Image
  Insha za hoja Insha za hoja ni insha zinazoelezea jambo fulani katika hali ya kujenga hoja ambazo zinatetea msimamo fulani alionao mwandishi wa insha hiyo juu ya jambo analolizungumzia. Hoja ni maelezo bayana yanayotolewa na mwandishi kutetea msimamo wake. Katika uandishi wa insha za aina hii, mwandishi hutakiwa kuonesha ni jambo gani ambalo analiunga mkono na ni lipi ambalo hakubaliani nalo. Ili hoja zote zipate kueleweka ni sharti zipangwe katika mtiririko wa mawazo ulio sahihi kiasi kwamba mtu aisomapo anapata kuelewa ni mada gani mwandishi anaijadili na ana msimamo gani kuhusu mada hiyo. Mambo ya Kuzingatia Katika Uandishi wa Insha za Hoja Unapoandika insha za hoja, au aina zingine za insha, zingatia mambo haya: 1. Kubaini mada ya kuandikia insha na kuielewa vyema. 2. Kupanga mawazo katika mtiririko wenye mantiki. 3. Kutumia mtindo unaoendana na kusudi la  insha . Kwa mfano, mtindo wa masimulizi, unafaa kwa hadithi au insha zingine za kisanaa. 4. Kutumia lugha fasaha na inayoelew